Kezastore

10006 – MANUFAA KUTOKANA NA HUDUMA ZA KEZASTORE (Kevin)

MANUFAA KWA MAKAMPUNI NA WASAFIRI KUTOKANA NA HUDUMA ZA KEZASTORE

Kezastore ni nini?

Hili ni swali ambalo umeruhusiwa kujiuliza kwa sasa, maanake ningali sijakuelezea Kezastore  ni nini na yakuhusu vipi.

Lakini niruhusu nianze kwa msemo ambao wahenga walituacha nao, ‘fuata maji yaendako’.

Ni dhahiri kwamba mambo yanapobadilika, nawe usikubali kuwachwa nyuma.

Kezastore ni tovuti itakayokuwa na huduma za kutuwezesha kukata tikiti za usafiri kwa kutumia mbinu za mkondoni.

Kwa kifupi unatembelea tovuti ya Kezastore, kisha kujisajili.

Kisha unaangalia ujumbe kuhusu njia zilizopo kutokana na mashirika ya kusafiri tofauti tofauti, ambayo itakusaidia kununua ama kukata tikiti yako.

Hivyo basi waweza kuitumia simu yako ambayo ni dijitali, ama vilevile kuitumia tarakirishi yako kuingia katika tovuti ile ndio kuweza kujisajili.

Kiungo cha huduma hii ndani ya tovuti ni: ticketing@kezastore.com

Huduma hii imetayarishiwa vikundi mbalimbali, toka makampuni, wasafiri binafsi, na kampuni za mabasi.

Changamoto zilizopo katika mfumo wa sasa

Mswahili alisema yakwamba, ‘Awashwaye ndiye ajikunaye’.

Sababu kubwa ya kubuni kuhusu mfumo wa kukata tikiti kutumia mtandao, ni shida tulizo nazo kwa sasa kama wakenya.

Misongamano ya watu na magari imekita mwendo masaa ya asubuhi na jioni, sanasana sehemu kama Githurai, upande wa Lang’ata na barabara ya Mombasa.

Hili linasababisha watu wengi kuchelewa kazini, wanabiashara kupoteza mikutano na wateja wao, na changamoto zingine mbalimbali.

Pia, serikali ya Kenya imepata changamoto kubwa kuhakikisha kwamba sheria za barabara zinafuatwa.

Hili laletwa na miungano ya magari ambayo sio halisi.

Hivyo basi inakuwa ngumu kwa serikali kufuatilia kesi za sheria kutofuatwa iwapo kampuni hizi hazina ofisi zake maalum ama wanachama wanaotambulika.

Ajali za barabarani pia zinaleta wasiwasi, ambazo hutokana na magari kwenda kwa mwendo wa kasi usiostahili, ama kubeba abiria Zaidi ya waliokubaliwa.

Iwapo matumizi ya tikiti za mtandao yatakumbatiwa, basi changamoto mingi zitaweza kuondolewa katika mfumo wetu.

Faida za Mfumo wa Tiketi Mkondoni

Ni kweli kwamba kila jambo huwa na wakati wake.

Basi huu ndio wakati wa kutembea kwa mwendo wa teknolojia, na pia kuzungumza lugha yake.

Mfumo wa tikiti za mkondoni upo hapa kutusaidia kwa njia mingi kama wakenya.

Moja wapo ya njia hizo ni,  mtandao kuwepo masaa ishirini na mane kwa siku saba za wiki.

Kwa hivyo waweza kukata tikiti yako kutoka mahali popote, wakati wowote

Waweza pia ukapata usaidizi wakati wowote kutokana na tikiti, iwapo kuna kasoro wakati wa kulipia ama kujisajiri.

Hivyo basi jambo hili linakuruhusu kupanga ratiba yako bila wasiwasi.

Faida nyingine kutokana na mfumo huu ni kwamba, hakuna pesa ambayo imeongezwa juu kugharamia tume.

Ukilinganisha na jinsi tunavyo kata tikiti pale Ambassador kwa magari ya KBS, utapata kuwa tume mbalimbali zinakata pesa hizi.

Aya basi, mambo ya tikiti mtandaoni yanakuondolea gharama hizo, kumaanisha ya kuwa waweza pangia safari ya sehemu zingine za nchi iwapo muda unakubali.

Faida ya tatu ni kwamba waweza ukapata usaidizi kutoka kwa wahudumu wa Kezastore mtandaoni kuhusu shida yoyote inayokukumba.

Ila tu usaidizi, wahudumu watakupa ujumbe Zaidi na kukuelimisha jinsi ambayo huduma zingine zinatumika hadi kuhakikisha umeelewa maagizo na mbinu zote.

Kuna manufaa mengine kama kupata tuzo la upunguzo.

Ni kweli kuwa kampuni mingi zinazohusika na huduma za tikiti mitandaoni  huwa wana huduma za kukuza mbalimbali kwa wateja wao.

Hivyo basi unaweza kubahatika na kulipa pesa kidogo iwapo upate siku ambayo kukuza imeanzishwa.

Hapo utaweza kuokoa senti kadhaa kufanyia vitu vingine.

Faida ambayo ni muhimu kabisa ni kwamba mteja anapewa jukumu la kujichagulia kiti.

Wengine wetu tunapenda viti vya mbele, wengine vya nyuma, wengine viti ambavyo vimekaribiana na dirisha, na ladha zingine mingi.

Ni jambo nzuri sana kwani unapokata tikiti yako mtandaoni utaweza kuona viti ambavyo vimebaki na kufanya uamuzi wako ukizingatia mahali upendapo.

Faida ya mwisho ni ile ambayo itafurahisha wateja wote, na aina zote za vikundi.

Ni dhahiri kwamba kumekuwa na msongamano wa watu kwa kila kituo cha magari.

Hii hupatikana sanasana asubuhi watu wanapoelekea kazini, na pia masaa ya jioni wanaporudi nyumbani kutoka kazini.

Wateja watakapoanza kukata tikiti katika mtandao, hivyo basi kila mteja atakuwa na wakati wake wa kufanya hili.

Yaweza kuwa siku kadhaa kabla ya kusafiri, ama masaa kidogo kabla ya kuanza safari.

Pia mteja ataweza kulijua gari lake na kituo chake kwa mapema.

Hitimisho

Kwa kukamilisha, Kezastore  yatuletea huduma ambazo twaweza kufikiria yakwamba hatuzihitaji kama wakenya kwa sasa, lakini tutakapoanza kuzitumia, ndipo tutaweza kujua maana yake kinagaubaga.

Kwa kufanya hivi, tutakuwa tumejinufaisha kama wakenya, na pia kusaidia nchi, kwa sababu serikali ya Kenya itakuwa na kazi rahisi ya kudhibiti sekta hii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Select your currency